Saturday, July 14, 2012


Mwalimu wa madrasa alivyonajisi
wasichana wanne, wavulana wawili  
NI WA MIAKA MIWILI HADI 10, SHEIKH AKEMEA ASEMA
MEZANI KWAKE YAPO MASHAURI SITA YA NAMNA HIYO

Fredy Azzah
MATUKIO yanayofanywa na baadhi ya binadamu, yanaweza kufanya waamini wa dini mbalimbali kuamini kuwa kiama kimekaribia.Kwa kiasi kikubwa vitendo hivi ambavyo vipo kinyume kabisa na ubinadamu, vinatekelezwa na wale waliotarajiwa kuvikemea, huku wakiwa wamejificha na kivuli cha vyeo vyao.


Tuesday, June 12, 2012

Nani atawasaidi watoto hawa wanaofanyiwa unyama wa kutisha ndani ya gereza la Segerea?

Fidelis Butahe
KATIKA hali isiyo ya kawaida watoto wenye umri chini ya miaka 18 wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali au waliohukumiwa huwekwa sehemu moja na watu wazima katika Gereza la Segerea,  jijini Dar es Salaam jambo ambalo limesababishia baadhi yao kuingiliwa kinyume na maumbile na kuharibiwa vibaya.Tuhuma hizo nzito dhidi ya magereza zilibainika wakati Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, ilipokuwa ikieleza mambo mbalimbali iliyoyakuta katika gereza hilo baada ya kufanya ziara, mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo ya Mambo ya Nje ulinzi na usalama inayoongozwa na Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.

Friday, May 25, 2012

Hatuyapendi maisha haya, jamii inatuonea!

Na Fredy Azzah

NI wazi kuwa chini ya jua hakuna mtu au binadamu yeyote anayependa kudhalilishwa, kila mtu angependa kufanya kazi halali ili awe na uhakika na kipato chake.Hivyo basi, ukilitambua hilo utakuwa na sababu ya kutumia jicho la tatu na kutafakari mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii.Baadhi ya watu ambao pengine jamii imekuwa ikiwaangalia kwa jicho ambalo nadiriki kusema siyo sahihi, ni wasichana pamoja na wanawake ambao huuza miili yao katika maeneo mbalimbali nchini.Watu wengi wamekuwa wakiwatupiwa lawama kutokana na shughuli hiyo wanayofanya,  kila siku wakipewa majina mbalimbali kama vile machangudoa, dada poa, malaya na mengine mengi.Wakati jamii ikilitazama hivyo kundi hili, kwa upande wao nao wanailaumu  jamii kuwa ndiyo iliyowafikisha hapo walipo.Hivi karibuni  katika mazungumzo na baadhi ya  wanawake hao wanaofanya shughuli hiyo katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, wengi wao wanasema kutelekezwa na familia zao ama waume zao, ndiyo sababu kubwa iliyowafikisha wengi wao hapo walipo.



Thursday, May 24, 2012

Women rapists land Zim man in ICU

By Kitsepile Nyathi

Harare. A Zimbabwean man is seriously ill in hospital after he was allegedly attacked by a gang of three women rapists. The man is believed to be the latest victim of semen hunters who have attacked hitchhikers across the country.

According to the state owned Herald newspaper, the 25-year-old victim was kidnapped by an unidentified man and three women who held him hostage for two days. It is alleged that the man was looking for transport from the eastern border city of Mutare last Wednesday. He was offered a lift by the four, who were travelling in a Mercedes-Benz car.

haya yanatendeka kwenye jamii zetu, jamani tupige vita hali hii

Uozeshaji wanafunzi, watoto wachanga unavyoshamiri Simanjiro

mmoja wa wanafunzi aliyefanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari baada ya wenzake watatua lofaulu nao kuolewa wote.


Fredy Azzah

“SISI ukiwa na mtoto wa kike tayari unahesabu utajiri, sasa ni mtu gani mjinga utakubali kufa na njaa umwache mtoto akamalize miaka saba shuleni,” anasema Elibariki Kisongo mkazi wa Kirun’gurun’gu.

Mzee huyu wa makamu ya miaka 70, anasema kuwa licha ya kuwa na wasichana 13 aliozaa na wake zake watano hakuna hata mmoja aliyesoma.

“We acha ujinga bwana, nikiwasomesha alafu watakuja kunisaidia nini,” anasema mzee huyo anayesema huwaoza watoto wake wakioneka wakubwa ingawa anashindwa kujua huwa wanakuwa na miaka mingapi.

Wanawake wa kimasai wanavyotaabika baada ya waume zao kumaliza ngombe, maelfu wazitoroka nyumba zao 


UTELEKEZWAJI wa watoto na wanawake, unatofautiana kulingana na maeneo na mila za jamii ya eneo husika.Katika maeneo ya mijini na hata kwenye baadhi ya Vijiji, utelekezwaji huu huwa ni wa kuwarudisha wanawake nyumbani kwao ama kuwafukuza na kwenda wanapojua.Lakini katika maeneo ya Masaini na hususani Simanjiro, hali ni tofauti, utelekezwaji unafanyika kwa wanaume kuondoka majumbani kwao na kuwacha wanawake na wakiendesha familia mbazo ni kubwa ama kuendelea kusihi nao lakini shughuli zote za familia wakiachiwa wao.
Ana Moreta (49) mkazi wa Kijiji cha Narokusoito kata ya Langai, ni mwathirika wa ulelekezwaji huo, ambapo sasa ana mzigo wa kuendesha familia yenye watoto nane baada ya mume wake kuondoka nyumbani na kwenda kusikojulikana.Kutokana na kutokuwa na mashamba wala mifugo, kwa sasa mama huyo analazimika kuendesha familia yake kwa biashaya ya kuuza ugoro na maziwa kidogo anayouza baada ya kamua Ngombe wake wawili.



Mila za Kimasai zinavyobariki ubakaji



Fredy Azzah

Katika Wilaya ya Sumajiro, suala la ubakaji wazawa wa eneo hili ambao kwa kiasi kikubwa ni wamasai na waarusha, wanasema lipo kwa kiasi kidogo na kwamba linaletwa sana na wahamiaji katika eneo hili.
Hata hivyo kauli za wazawa wa eneo hili zinakinzana na zile za baadhi ya watendaji wa serikali na wananchi wasiyo katika eneo hili wanaosema ubakaji ni mkubwa.
Hata hivyo vitendo vya ubakaji vinaonekana kutoripotiwa kwa wingi katika polisi, ingawa vinaelezwa kutendeka.
Kwa mujibu wa taarifa za Wilaya ya Sumanjiro, kwa mwezi kunaripotiwa matukio kati ya matatu mpaka matano.
Wengi wanaoeleza kuwepo kwa matukio hayo kwa wingi, wanasema yanafanyika sana katika ngoma ya kimasai inayoitwa Esoto.

“Ukiniambia nieleze ukubwa wa tatizo la ubakaji katika jamii ya Simanjiro nitakuambia ni karibu asilimia 90 ya watoto wanabakwa,” anasema Mtendaji wa Kata ya Endonyongijape Mary Chisoji.


Simanjiro waanza kukeketa watoto wachanga, Madaktari wasema madhara zaidi yataongezeka
Huyu ni ngariba aliyekeketa maelfu ya wasichana katika eneo hilo

Fredy Azzah

WAKATI serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka ndani nan je ya nchi yakitafuta njia ya kupambana na ukeketaji, ndivyo jamii inayoabudu mila hizi potofu wanavyotafutwa njia ya kutekeleza ukatili huo bila kubainika.
Jamii ya wananchi wa Simanjiro ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wamasai na waarusha, wamebadili kutoka kufanya ukeketaji kwa wasicha wenye umri mkubwa uliokuwa ukikadiriwa kuwa 14 mpaka 18 na sasa ni watoto  wadogo wenye wiki moja mpaka mwezi mmoja.

Nang’urutu Kariayi (49), mkazi wa Narokusoito kata ya Langai, ni ngariba maarufu katika eneo hilo ambaye alianza kazi yake hiyo zaidi ya miaka 10 iliyopita, anathibitisha hilo akisema kuwa lengo kuu ni kukwepa kukamatwa na kuweza kulinda mila za kabila hilo.

 “Kwa siku nakata hata zaidi ya 10 kwa sababu kwa mtu mmoja anaweza akawa ana mabinti watano, na ile kitu siyo ngumu kwa sababu haina mfupa,” anasema Kariaya baada ya kutaka kujua idadi ya watoto anaowakeke kwa mwaka.