Saturday, July 14, 2012


Mwalimu wa madrasa alivyonajisi
wasichana wanne, wavulana wawili  
NI WA MIAKA MIWILI HADI 10, SHEIKH AKEMEA ASEMA
MEZANI KWAKE YAPO MASHAURI SITA YA NAMNA HIYO

Fredy Azzah
MATUKIO yanayofanywa na baadhi ya binadamu, yanaweza kufanya waamini wa dini mbalimbali kuamini kuwa kiama kimekaribia.Kwa kiasi kikubwa vitendo hivi ambavyo vipo kinyume kabisa na ubinadamu, vinatekelezwa na wale waliotarajiwa kuvikemea, huku wakiwa wamejificha na kivuli cha vyeo vyao.



Mmoja wa watuhumiwa wa vitendo hivyo ni Ismail Islam Mohamed ambaye ni mwalimu wa madrasa iliyopo Mtaa wa Masulize Twangoma Temeke jijini Dar es Salaam, ambaye anadaiwa kubaka watoto wanne na kulawiti wengine wawili.
Wazazi wa watoto waliofanyiwa vitendo hivyo ambao pia ni wanafunzi wa chekechea na shule ya msingi iliyopo katika eneo hilo, wanasema Mohamed alitekeleza vitendo hivyo kwa nyakati tofauti na kuwa aliwahi kuhojiwa mbele ya wazee msikiti na kukana kutenda vitendo hivyo.
Wazee wa msikiti huo, wanasema Mohamed aliwaambia kuwa watu wa eneo hilo wanamsingizia vitendo ambavyo hajawahi kuvifanya.
Hata hivyo, wakazi wa eneo hilo wanasisitiza kuwa amekuwa akitenda vitendo hivyo kwa nyakati tofauti, hivyo kuamua kuripoti suala hilo polisi ambako amefunguliwa faili na huenda likafikishwa mahakamani.

Malalamiko ya wazazi
Mmoja wa kinamama ambao watoto wao walnadaiwa kubakwa na  ambaye jiana nalihifadhi kwa kuzingatia maadili anasema mwanae wa miaka mitano alifanyiwa kitendo hicho.Anasema mwanae alikuwa hajaribu kueleza unyama aliotendewa hadi alipomshuhudia akiwa ametapakaa usaha  kwenye nguo za ndani.“Kama wiki mbili zilizopita, kila nilipokuwa nikifua nguzo zake za ndani, nilikuwa nikizikuta na usaha, siku ya kwanza ilibidi nimchape aniambie ni kwa nini, hakusema. Nikamuacha.  kesho yake nilipokuta ile hali ilibidi nimtishie kama vile namchoma na moto,” anasema na kuongeza:
“Hapo sasa ilibidi anieleze hali ilivyokuwa. Aliniambia wakati wakienda Madrasa, muda wa msikitini ukifika mwalimu wake humkataza kwenda msikiti na kumwambia yeye na wenzake watatu wafagie  banda la kuku ama kufanya usafi hapo walipokuwa wanasomea.”
Anasema nyakati hizo ndozi mdaiwa alizitumia kutenda uovu dhidi ya watoto hao, ambao walikuwa wakimuamini pia kumuogopa, hata kufikia kumfichia siri.
Mmoja wa watoto hao, anasema wakati wenzao wakielekea msikiti, mwalimu huyo alikuwa anawaambia wavue nguo za ndani kisha kuwaingizia vidole na umme kwenye sehemu zao za siri na sehemu ya kutolea haja kubwa.
“Ustadhi tukienda msikitini anatuvua nguo za ndani mpaka kwenye magoti, anatuambia  tupige magoti halafu anatuingizia vidole na dudu yake,” anasema mtoto huyu kwa aibu huku akiwa ameziba uso wake viganja vya mkono.
Anasema kwamba, hawakuthubutu kuwaeleza wazazi wao kwa sababu, mwalimu wao huyo aliwaambia wakifanya hivyo atawachapa.
Naye mzazi mwingine, ambaye mtoto wake ana miaka miwili na nusu, anasema baada ya kugundulika kuwa mtoto wa kwanza amefanyiwa hivyo, naye alishirikishwa kwa kuwa mtoto wake anasoma kwa mwalimu huyo.
Anasema kuwa kabla ya tukio hilo kubainika, kama majuma mawili nyuma mtoto wake alikuwa anashindwa kujisaidia haja kubwa na ndogo, jambo lilipompa wasiwasi na hivyo kumshirikisha mama wa jirani yake ambaye alimshauri kumpa mtoto matunda.
Mama huyu anasema hali ilizidi kubadilika na mtoto alikuwa analia sana hata pale alipokuwa akiogeshwa, jambo lililompa mama yake wasiwasi zaidi ingawa hofu juu ya kuwa kuna mtu anamwingilia haikuwepo kwa kuwa katika eneo hilo hakuna watoto wa kiume.
“Nilipata wasiwasi nikamuuliza mtoto akienda madrasa huwa anafanyiwa nini, akaniambia mwalimu wake huwa anamvua nguo na kumwingizia vidole,” anasema mama huyo.
Mama huyu anasema pia kuwa, mtoto wake mwingine mwenye miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa mwalimu huyo, alipohojiwa alisema ni kweli kuwa mwalimu huyo huwa anawabaka.
Mtoto wa miaka miwili na nusu, naye anasema: “Ananivua nguo, ananiambia njoo huku, ananipiga huku na vidole,” mtoto huyo ambaye hajui kuzungumza vyema anasema.
 Mtoto wa miaka 12 anasema: “Alikuwa ananivua nguo zote ananichapa huku akiniambia ananipa adhabu kwa kuwa mama amemwambia naibia hela nyumbani. Akimaliza kunichapa ananishikashika maziwa huku akiniingizia vidole nyuma (sehemu ya haja kubwa) na ume wake,” anasema.
Anasema kwamba mwalimu huyo amemfanyizia kitendo hicho mara nyingi ambazo hawezi kumbuka idadi yake. Mara zote, anadai alimtishia kwamba akisema nyumbani atamchapa zaidi pia na kumtahadharisha kusema hivyo hivyo ni dhambi.
“Wakati mwingine anatuambia tukisema atatusomea dua tufe,” analalamika mtoto huyo.
Mzazi mwingine, ambaye mwanaye ana miaka sita, anasema kuwa Julai 7 mwaka huu ndipo alipogundua kwamba mwanae anafanyiwa vitendo hivyo baada ya wenzake hao kubainika.
Anasema baada ya kumhoji mtoto wake alikiri kuwa mwalimu wake huwa anamfanyia vitendo hivyo jambo ambalo lilimshitua.
 “Mwalimu alikuwa anatuambia tuvue nguo anatuambia tupige magoti, halafu yeye anatuingizia vidole na dudu lake” anasema mtoto huyo.
Mzazi mwingine anasema baada ya kubaini suala hilo walikusanyana na kufanya kikao ambacho waliafikiana kwenda polisi ambako walifungua faili la malalamiko na kupatiwa hati ya kwenda kupata matibabu.
“Tarehe saba (Julai, mwaka huu) ndiyo tuligundua haya, Jumapili tukawapeleka watoto hospitali ya Temeke wakapimwa wawili walikutwa na uchafu sana na wengine walionekana wameingiliwa lakini hawakuwa na uchafu,” anasema na kuongeza:
“Tulipotoka hapo tulipitia polisi Mbagala wakatupa askari tuje kumkama, tulivyofika kwao hatukumkuta mpaka leo anatafutwa. Haijulikani alikojificha,” anasema mmoja wa wazazi.
Wakazi wa eneo hilo pia wanalalamika kuwa mwishoni mwa mwaka jana, mtuhumiwa alishtakiwa kwa wazee wa msikiti kwa madai ya kulawiti watoto wawili wa kiume.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikana lakini wazee walikuja juu na kumuonya kutokana na watoto wanaodai kutendewa kitendo hicho kusisitiza kuwa ni kweli walifanyiwa vitendo hivyo.
Utata juu wa mtuhumiwa
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, hawaelewi hasa kijana huyo ni mtu wa wapi licha ya kuishi katika eneo hilo kwa takribani miaka mitatu sasa.
“Sisi  tunajua tu kuwa huyu jamaa katoka Mombasa,” wanasema watu wa eneo hilo.
Mwenyekiti wa msikiti wa eneo hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake, anasema kamwe tukio hilo lisihusishwe na dini na kuwa hiyo ni tabia ya mtu mwenyewe.
Anasema kwa muda aliomfahamu Ustadhi huyo, hata siku moja hakujua kwamba anaweza kuwa na tabia kama hiyo.
“Nasikitishwa sana na kitendo alichofanya,” alisema Sheikh huyo aliyesema dini ya Kiislamu inakataza na kukemea vikali matendo hayo.
Majirani
Yunusi Mosha (45) na Maneno Salum (41) ni wakazi wa eneo hilo na walifikiwa na fununu za matukio hayo. Wao wanaonya vikali na kutaka jamii ya eneo hilo kukemea vitendo hivyo kwa kushirikiana na kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa kwenmye vyombo vya sheria.
 “Hii hali imekuwa ikinipa wasiwasi, kwa sababu siyo jambo la kawaida mwanafunzi anamuona mwalimu wake anakimbia na kujificha,” anasema Mosha.
Mwenyekiti wa mtaa wa Twangoma,   Mohamed Chande anasema kuwa taarifa za tukio hilo alipewa Mtendaji wa Mtaa huo John Mgaya ambaye hata hivyo hakuwepo ofisini.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Amaan Malima anasema taarifa za daktari aliyewapima watoto hao bado hazijamfikia lakini akasema wakati mwingine siyo rahisi kutolewa hadharani hadi wahusika watakaporuhusu.
Polisi wamtafuta
Kwa upande wa Kamanda wa polisi Wilaya ya Temeke, David Misime anasema tukio hilo liliripotiwa polisi Mbagala na kuhifadhiwa kwa RB namba 6549/2012.
Anasema mtuhumiwa yaeleka alipata taarifa mapema hivyo akatoroka na polisi wanaendelea kumsaka.
 “Askari walienda ili kumkamata lakini hawakumkuta. Hili tukio nalifuatilia kwa ukaribu sana hata jana tu niliuliza juu ya uchunguzi wake unavyoendelea,” anasema Kamanda Misime.
Mbali na tukio hilo, alisema kuna mengine mawili ya aina hiyo ndiyo anayoyakumbuka na uchunguzi wake pia unaendelea.
Sheikh wa Mkoa asema
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa anasema analaani sana tukio hilo kwani linachafua jina la walimu wa dini hiyo ya Kiislam nchini.
Musa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Madrasa Tanzania anasema mbali na tukio hilo, ofisini kwake ana malalamiko sita ya matukio ya namna hiyo.
“Hawa ni watu ambao kwa kweli hawakustahili kuwa walimu wa dini. Tumekuwa  tukifanya mikutano na semina ambapo huwa tunazungumza sana haya mambo, nadhani hii ni watu kukosa maadili,” anasema Sheikh Musa.
Naye, Mkurugenzi wa Tamwa, Ananilea Nkiya anasema vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinaendelea kushamiri nchini na kuonya ni lazima vikemewe kwa nguvu zote na jamii nzima.
“Polisi wahakikishe wanamkamata huyo mtu na afikishwe kwenye vyombo vinavyo. Inasikitisha sana mtu anaharibu watoto kiasi hicho,” anasema.
Dada wa mtuhumiwa ambaye ambaye hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kile alichodai katika dini ya Kiislam mwanamke haruhusiwi kuzungumza bila idhini ya mumewe anasema tukio hilo limemwibulia simanzi.
“Sijui alipo. Aliondoka Jumapili asubuhi akisema tutamtafuta hatutampata... Kinachonisikitisha ni kwamba alipokuwa anafundishia ni karibu sana na chumbani kwangu. Hapa nilipo nimechanganyikiwa,” alilalamika.
MWISHO 

No comments:

Post a Comment